RAIS John Magufuli amemtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Marekani, Donald Trump ambaye aliibuka mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, uliofanyika jana na hivyo kumfanya kuwa Rais wa 45 wa taifa hilo kubwa lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kijeshi.
Katika salamu zake kupitia anuani yake ya mtandao wa Tweet, Dk Magufuli aliandika, “Hongera Rais mteule Donald Trump na watu wa Marekani. Mimi na Watanzania tunakuhakikishia kuendeleza urafiki na ushirikiano wetu.”
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi