Mgogoro mkubwa umeibuka baina ya wananchi wa
kijiji cha Missiwa kilichopo katika kata ya Ipelele tarafa ya Magoma wilayani
Makete baada ya mama aliyejulikana kwa jina la Merry Mwamande kupewa idhini na
mahakama ya mkoa wa Njombe kuendelea kuuvuna msitu ambao kijiji hicho kinadai
kuwa kinaumiliki kihalali.
Hayo yamebainika wakati wa mkutano kati ya
uongozi wa kata ya Ipelele na wananchi wa kijiji hicho uliofanyika katika ofisi
ya kijiji cha Missiwa baada ya kusomwa waraka uliotoka mahakamani kuwa mama
huyo aitwaye Merry Mwamande ameshinda kesi hivyo kupewa kibali cha kuendelea
kuuvuna msitu huo.
Kwa mujibu wa maelezo ya baadhi ya wananchi na
viongozi wa kijiji hicho wanadai kuwa mwaka 2006 waliwahi kuuza msitu huo kwa
ajili ya ujenzi wa shule lakini eneo lilibaki kuwa miliki ya kijiji hicho
lakini wanashangaa kuona mama huyo anaposema ni eneo lake.
Pia taarifa kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho
zinadai kuwa lilipofunguliwa jalada kuhusu kesi hiyo wananchi walikuwa
wakichanga fedha na kumkabidhi mwenyekiti mstaafu anayeitwa Bw.Lingison Mbwilo
ili aweze kuhudhuria kesi hiyo lakini inasemekana alikuwa haendi hivyo mahakama
ikaamua kuwa eneo hilo apewe mama huyo jambo ambalo wananchi na baadhi ya
viongozi wa kijiji hicho wanalilalamikia.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mpya wa kijiji cha
Missiwa aliyechaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana
Bw.Mesaukyadi Mbola akaelezea namna alivyokabidhiwa ofisi hiyo.
Kwa upande wake Mama anayelalamikiwa
aliyejitambulisha kwa jina la Merry Mwamande ambaye anaishi Ntokela wilayani
Rungwe akaelezea kuhusu madai hayo.
Pia ameongeza kuwa anashangaa kuona wananchi wa
kijiji hicho wanalalamikia maamuzi ya mahakama kwani walipoitwa mahakamani
walikuwa hawafiki.
Diwani wa kata ya Ipelele Mh.Mwipelele Mbogela
amezungumza na kituo cha redio Green fm mara baada ya mama huyo kuzungumza na mwandishi wetu na
kudai kuwa msitu huo ni wa kwake na kudai kuwa haafiki anachokisema mama huyo
huku akieleza hatua atakazochukua kama diwani.
Na Fadhili Lunati
Na Fadhili Lunati
Sikiliza sauti hizi hapa chini:-