Askari Polisi watatu wafukuzwa kazi Mwanza

Jeshi la polisi mkoani MWANZA limewafukuza kazi askari  watatu kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya uhalifu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa MWANZA, AHMED MSANGI amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa na jeshi hilo ili iwe fundisho kwa askari wengine ambao hawazingatii weledi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumza na Watendaji wa Jeshi la polisi mkoani MWANZA wakati wa kikao  cha kazi kilichofanyika kufuatia ongezeko la matukio ya ukiukwaji wa maadili miongoni mwa baadhi ya Watendaji hao, Kamanda MSANGI amesema vitendo hivyo havivumiliki.

Kamanda MSANGI ametumia kikao hicho kuwakumbusha Watendaji wa Jeshi la Polisi mkoani MWANZA kuzingatia weledi wakati wa kutekeleza  majukumu yao na kufanya kazi zao bila kumuogopa wala kumuonea mtu yoyote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo