Moja ya habari ambazo zimetawala katika mitandao mingi ya kijamii kwa Alhamisi ya Novemba, 3 ni habari ambayo inamhusisha model aliyetumika katika wimbo wa Diamond Platnunz na Rayvanny – Salome kuwa amepoteza maisha kufuatia kutekwa, kubakwa na kuuliwa kisha mwili wake kutupwa mtaroni.
Taarifa iliyokuwa katika mitandao imemtaja model huyo kuwa jina lake Juliana lakini kipindi cha XXL cha Clouds Fm kimemtafuta model huyo na amekanusha kuwa sio yeye ambaye amefariki na jina lake sahihi ni Lillian na ameshtushwa na habari hizo kwani hamfahamu hata mtu aliyekutwa na mkasa huo.
Sikiliza sauti hii hapo chini:-