Mwanaume mmoja nchini Kenya ajinyonga akihofia ujauzito wa mkewe kuharibika tena.
Mwanaume mwenye umri wa miaka 27, Antony Juma wa nchini Kenya amejiuwa kwa kujinyonga kwa kuhofia kuwa mke wake ambaye ni mjamzito, mimba yake ingeharibika tena.
Awali mke wa Antony Juma, ujauzito wake ulishaharibika mara mbili, na hofu ya ujauzito kuharibika tena ilimfanya kujinyonga kwa kamba kwenye nyumba ya kupanga katika kaunti ya Homa Bay.
Mwili wa mwanaume huyo ulikutwa ukining'inia kwenye paa la nyumba na mkewe ambaye alienda kumuita ili aende kufanya shughuli zake za nyumbani za kila siku.
Mdogo wake wa kiume, Jared Juma, amesema kaka yake alikuwa ameathirika mno kisaikolojia kutokana na matukio ya mkewe kuharibu ujauzito.