Godbless Lema akiwa na Mkewe, Neema Lema
Akimsomea mashitaka hayo kwa mara ya kwanza, Wakili wa serikali Blandina Msawa, mbele ya hakimu Agustino Rwezile, alidai kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha alimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani Mkuu huyo wenye lugha ya matusi Mkuu huyo, huku akijua ni kosa kisheria.
Alidai mtuhumiwa huyo alituma ujumbe kutoka 0764150747 namba 0756551918 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”
Mrisho Gambo - Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mshitakiwa alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena kesi hiyo.
Hata hivyo baada ya kuachiwa huru nje ya Mahakama, Neema alisema anashanga kuunganishwa katika kesi hiyo, lakini yeye hajamtukana Mkuu wa Mkoa, japo simu ni yake ilitumika kama wanavyodai kutuma ujumbe huo.
“Mimi wanadai nimemtumia meseji za matusi katika simu ya Gambo na sijamtukana Mrisho Gambo, ila kwa kuwa simu ni mali yangu, hivyo niko tayari kupambana na Mrisho Gambo na mimi nawasiliana na Mrisho Gambo na sio kwa mara ya kwanza, ila tunawasiliana sielewi kwa nini hii achukulie matusi,”alisema.
Mbunge Godbless Lema
Mbunge Godbless Lema, alisema anashukuru mke wake anapita kwenye mambo anayopitia na itamfundisha ujasiri wa kuomba vizuri na tangu awe na matatizo mke wake hajawahifikishwa amahakamani na yeye siku hiyo ni Baraka kubwa kwake.
“Ila nilitamani aende akajue magereza ipoje kwa kukaa siku 14 magereza ila madiwani wamenishauri sana nikaona tumdhamini tu, ila ushoga sio jambo baya, ila tutamshinda na tutamdhibiti gambo na tunaamini haki yetu tutaipata mahakamani,”alisema.