NJOMBE.
Wakazi Wa wilaya ya Wanging'ombe
mkoani Njombe wameiomba serikali kuwasogezea karibu huduma ya kituo cha afya
ili baadhi ya wanaume ambao hawajafanyiwa
tohara waweze kupatiwa huduma hiyo kwani baadhi yao wamekuwa wakidai
huduma zipo mbali hivyo wanashindwa kufika huko.
Ombi hilo limeombwa na baadhi ya wanaume ambao hawajafanyiwa tohara
katika kijiji cha Itowo kata ya Mdandu wilayani Wanging'ombe ambao
wamemweleza mhamasishaji wa eneo hilo
kuwa wanashindwa kwenda kufanyiwa tohara kutokana na umbali uliopo hadi kufika
katika hospitali ya Kibena Njombe ambako huduma hiyo pia inapatikana.
Akizungumza na mwandishi wa Green Fm Grace Sanga, mmoja wa waelimishaji hao amesema kuwa hivi sasa
muamko wa wanaume kwenda kufanyiwa tohara umekuwa mkubwa kutoka na elimu
inayoendelea kutolewa kwa wanaume kuhusu faida na hasara za kutofanya tohara.
Pia imeelezwa kuwa kumekuwa na baadhi ya
changamoto mbalimbali kwa baadhi ya wanaume kama vile kuogopa kufanyiwa tohara kipindi
cha msimu wa joto kwa Imani kuwa vidonda vitachelewa kupona, na wengine
wakiamini kuwa baada ya kufanyiwa tohara nguvu za kiume zitapungua hivyo kuwafanya washindwe
Hivyo wanaume ambao bado
hawajafanyiwa tohara wametakiwa kuachana
na Imani potofu na kushauriwa kuchukua hatua ili kujikinga wao pamoja na
wenza wao na maradhi yanayosababishwa na kutofanyiwa tohara.
Na Grace Sanga