Wananchi wa kijiji cha Usililo kilichopo kata ya Luwumbu
wilayani Makete mkoani Njombe wameaswa kuwa mstari wa mbele katika kufanya
shughuli za kimaendeleo ili kukiinua kijiji hicho ikizingatiwa bado kiko nyuma
kimaendeleo.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii Asukile Mwalwembe, Afisa Mtendaji wa kijiji hicho
Bi Victoria Sangu amesema wanamikakati mingi katika kuhakikisha wanapiga hatua
kimaendeleo na kuomba wananchi wampe ushirikiano.
Pia Afisa mtendaji huyo amesema kuwa kama wananchi wa
kijiji hicho wataendelea kutoa ushirikiano watakisogeza mbele kijiji chao na
kuomba waandishi wa habari kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa hamasa kwa wananchi
hao kujitokeza katika shughuli za maendeleo.
Bi Sangu amesema kuwa wananchi wengi wa kijiji hicho cha
Usililo wanajitokeza kwa wingi Kushiriki shughuli za maendeleo licha ya baadhi
ya watu kutojitokeza ingawa wanawachukulia hatua na kuongeza pia hawaingizi
itikadi za kisiasa katika kufanikisha suala la maendeleo.
na Asukile Mwalwembe