"Wanafunzi acheni Kuwapiga walimu Wenu" asema Meya Mwita

NA MWANDISHI WETU, Dar
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka wanafunzi kuwaheshimu walimu na kuacha tabia ya kuwapiga kama ambavyo inavyo jitokeza kwa sasa katika maeneo mbalimbali kutokana na kile alichoeleza kwamba hatua hiyo ni utomvu wa nidhamu.

Aidha Meya Isaya ameonesha kuchukizwa na mavazi ya watoto wa kike na wakiume na hivyo kuwataka wazazi kusimamia ili kuliepusha taifa kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili.

Meya Isaya aliyasema hayo jiji hapa wakati wa mahafali ya dini ya Umoja wa Katoliki (TYCS) , na mashirika ya kipentekoste (UKWATA) katika shule ya sekondari Green Agres iliyopo Mbezi bichi.

Alisema siku hizi kumeibuka matukio ya wanafunzi kuwapiga walimu wao jambo ambalo alisema ni ukosefu wa maadili na kwamba mwalimu anapaswa kuhesmiwa kwakuwa ni mzazi wa pili kwa mtoto.

Alisisitiza kwamba, hatua ya mwanafunzi kumpiga mwalimu inaonyesha ishara ya wanafunzi kushindwa kusoma na kwamba huenda taifa likakosa wasomi makini kama jambo hili halite angaliwa kwa macho ya upana.

“Mwanafunzi unapompiga mwalimu unakusudia nini, hivi karibuni tuliona kwenye vyombo vya habari, wananfunzi wamewacharaza bakora walimu wao, sasa tunataka kwenda wapi, jambo hili nilakusikitisha lazima tulikemee kwa nguvu zote” alisema Meya Isaya.

Akizungumzia mavazi watoto wa kike na wakiume ,Meya Isaya alisema, anasikitishwa kuona namna ambavyo watoto hao wana vaa nguo na kutembea barabarani na hususani wanafunzi na hivyo kuwataka wazazi kusimamia jambo hilo kwa ukamilifu.

Alisema “iwapo mwanafunzi anamalia elimu ya sekondari lakini hana tabia ya kuvaa vizuri kama tunavyoona kwa watoto wengi kwa sasa, ni zahiri kwamba tunatengeneza kizazi cha nyoka badala ya Taifa, kama yasemavyo maandiko matakatifu.

Alifafanua kwamba , kila moja anapaswa kuwa na madili mema kutokana na kwamba serikali imewekeza zaidi kwenye elimu ili kupata kizazi ambavyo kimesoma na kuweza kuliongoza Taifa.

“ Sikuhizi dunia imebadilika, vijana hawana maadili kabisa hasa kwenye mavazi, wanaiga mambo ya kwenye mitandao ambayo hayana faida kwenu, nikiwa kama baba yaenu, kiongozi wenu, msisige mambo ya dunia, hayata wafikisha popote” alisema Meya Isaya.

“Mnafanya mambo haya kwa sababu mnashindwa kuvumilia, mnataka mambo makubwa ndio mana mnavaa mavazi mabaya, nikipita na kutana na watoto ambao wana umri wa kusoma lakini mavazi yao hayana maadili, wazazi mnataka kulipeleka wapi Taifa?” aliwaluliza wazazi ambao walihudhuria sherehe hiyo.

Alisema katika kuhakikisha kwamba watoto wanarudi kwenye mstari mzuri, wazazi hawana budi kuwa wakali katika hilo, na hata walimu kuweka sheria shuleni ili kunusuru taifa mabalo serikali inawekeza kwa nguvu kubwa kwenye suala zima la elimu.
 
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Ntipoo Reco alisema kwamba mbali na kumshukuru Meya wa jiji kufika katika mahafali hayo, aliwataka wahitimu hao kuziangatia maelekezo yake ili waweze kufanikiwa vizuri kwenye masomo yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo