Meya wa jiji la Dar atoa maneno mazito kwa familia ya Dk. Masaburi

NA MWANDISHI WETU, Dar
MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ameiomba familia ya aliyekuwa Meya wa Jiji Dk. Didas Masaburi kuwa pamoja katika kipindi hiki kigumu na kuachana na mambo ya chuki ambayo yanaweza kuisambaratisha familia.
  
Aidha  Meya Isaya  aliahidi kuendeleza mambo mazuri ambayo Dk. Masaburi aliwahi kuyafanya pindi alipokuwa kwenye nafasi hiyo na kwamba wananchi wa Dar es Salaam waendelee kumuenzi kwa mema ambayo aliyafanya.


Meya Isaya aliyasema hayo jana jijini hapa wakati wa kumuaga marehemu Dk. Masaburi ambapo ibada hiyo ilifanyika katika viwanja vya karimjee na badae kuelekea Shambani kwake Chanika kwa ajili ya mazishi.

Alisema anatambua familia ipo katika kipindi kigumu cha  maombelezo lakini jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba wanaishi katika maisha ya furaha na upendo na kuacha mambo ya Ubaguzi ambayo yatasababisha kusambaratisha familia yao.


"  Jamani msiba ni jambo zito sana, poleni, lakini ninacho waomba ,mpendane, mshirikiane,  endelezeni furaha ambayo alikuwa anawapa baba yenu wakati wa uhai wake, wakubwa muwapende wadogo zenu, "alisema Meya Isaya.

Akimzungumzia Dk.Masaburi Meya Isaya alisema anatambua mambo makubwa ambayo aliyafanya wakati  alipokuwa kwenye nafasi hiyo ikiwemo kupigania kuwepo kwa kipengele cha ugwatuaji wa madaraka kwa serikali za mitaa kwenye katiba Mpya.

Alisema jambo hilo limewezeshwa hata sasa serikali za mitaa kuwa na mamlaka tofauti na ilivyo kuwa awali kwani hivi sasa mbali na kwamba katiba Mpya bado haija pita lakini serikali za mitaa zina mamlaka ya kufanya mambo ya maendeleo kwa wananchi.

Mbali na hilo, Meya Isaya alisema atamkumbuka Dk.Masaburi kutokana na juhudi zake za kupigania uboreshwaji wa miundombinu ya jiji ambayo ilikuwa ikifadhiliwa chini ya benki ya dunia.

Alisema " sio hayo tu, ameweza pia kuunganisha jiji la Dar es Salaam na majiji mengine ambapo imekuwa ni rahisi kwangu kutambulika na kufanya mazunguzo ya maendeleo na miji mingine, leo hii ukipita kwenye maeneo mbalimbali utakuta vibao ambayo vimeandikwa majina ya mji wa Humbager ikiwa ni sehemu ya kuboresha mahusiano na Ujerumani .

Sasa,  kwa nafasi yangu, nitaendeleza yote mazuri , ikiwa ni njia moja wapo ya kumuenzi mtangulinzi wangu huko alipo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo