Mbatia ataka Uhakiki wa vyeti feki uanzie kwa Rais na viongozi wengine


Mhe. James Mbatia (MB) Vunjo, na Mwenyekiti Taifa NCCR Mageuzi Ametaka zoezi la uhakiki wa vyeti feki ni vyema likanzia kwa Rais na viongozi wengine.

Binafsi jamii forums inaunga Mkono hoja ya Mhe.Mbati kwa sababu mbili tu.

1.Kiongozi hutakiwa kuongoza kwa Mfano, tulitegemea akianza Rais, watafuata na viongozi wengine wote, PM, VP, W. N/W, RC, DC, Wabunge hadi Madiwani.

Aidha, kuna mazoezi mengi hapo awali yalianzishwa na Rais na viongozi wengine Tuliona wakati wa kampeni mbalimbali kama vile UKIMWI na Malaria No More, Tuliona Utambulisho wa anuani za makazi, Tuliona kwenye BVR na NIDA.

Ikumbukwe kuwa, JPM alikuwa mastari wa mbele, kwa maana wa kwanza katika Zoezi la UHAKIKI WA SILAHA Mkoa wa Dar.

2. Kuonyesha uhalali wa zoezi husika, kuwa kama zoezi likianza na Viongozi mara nyingi huchukuliwa ni 'serious' na ni zoezi halali lisilo la kibaguzi kwa baadhi ya kada tu.

Kwani Mpaka sasa kuna baadhi ya Mawaziri inasemekana wanatumia majina fake, so uhalali wa zoezi hili upo wapi?

Zoezi lianze kusafisha Nyumbani kwanza ( Baraza la Mawaziri & vigogo)

Source: Jamii Forums


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo