Maiti yageuka FISI baada ya watoto kukosea masharti ya Kuizika

October 5, 2016 kupitia Leo Tena ya Clouds FM, Mtangazaji Geah Habib amekutana na stori huko Mtwara juu ya mwanaume mmoja aliyekua mganga wa kienyeji, mtu huyo inadaiwa kuwa alitoa masharti kwa watoto wake kwamba siku akija kufa basi mwili wake usitolewe kupitia mlangoni badala yake wavunje ukuta na kisha azikwe na nguo nyeusi.
Inasemekana kwamba baada ya kufariki watoto wake hawakutekeleza suala hilo na ndio jambo linatajwa kuwa limesababisha akageuka kuwa fisi ambaye anasumbua watu na kula mifugo kila wakati.
>>>>Kwa taarifa zilizopo kuhusu anakotokea huyo fisi wanadai alikuwa mganga wa kienyeji na alitoa masharti akisema siku nikifa mnizike bila sanda mnivishe nguo nyeusi, mbomoe ukuta ndo mtoe maiti msinitolee mlangoni sasa inadaiwa kuwa wale ndugu zake hawakufanya alivyotaka ndio ikatokea, nafikiri kuna mambo ya kiimani kwamba alitoka akaenda maeneo ya likondwe, mkunwa mpaka maeneo ya dihimba huko amefanya vurugu zake ndio karudi huku kwetu:- Shuhuda
Sikiliza full stori kwa kubonyeza Play hapa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo