Heeee Kimenuka Tena CUF...Lipumba na Jaji Mutungi Washitakiwa


Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF) leo imefungua Shauri Na. 75, 2016 katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi na Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na watu 12 waliosimamishwa uanachama wa chama hicho.


Wakili aliyefungua shauri hilo, Juma Nassoro ameuthibitisha kuwa, shauri hilo limefunguliwa na kwamba litasikilizwa rasmi Oktoba 10, 2016.



“Bodi ya Wadhamini CUF imefungua shauri dhidi ya Jaji Mutungi na wengine 12 waliosimamishwa uanachama pamoja na Lipumba,” amesema.



Amesema lengo la bodi hiyo kufungua shauri hilo, ni kuitaka mahakama kutoa amri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kutoendesha shughuli zake za usimamizi wa vyama vya siasa chini ya sheria za vyama vya siasa kwa madai kuwa hazimpi mamlaka ya kufanya hivyo.



“Tunatambua kuwa kesi kama hii ilishawahi tokea kwamba mahakama kuu ilitoa hukumu dhidi ya msajili wa vyama vya siasa kuwa hana mamlaka ya kuingilia mambo ya utawala wa ndani katika vyama vya siasa,” amesema na muongeza.



“Lakini sasa tunaitaka mahakama iende mbali zaidi, itoe amri ya kumzuia msajili kufanya shughuli zake ambazo ziko nje ya mamlaka aliyopewa na sheria za vyama vya siasa. Ili kuimarisha demokrasia na msajili kufanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria.”



Nassoro ameuambia mtandao huu kuwa, wajumbe saba wa Bodi ya Wadhamini CUF ambao amedai kuwa wanatambuliwa na msajili wa vyama vya siasa ndio waliomtaka kufungua shauri hilo.



“Wajumbe waliokuja kwangu ni saba, majina yao sina kwa sasa, hao wengine mnao wasikia wanaitisha vikao Buguruni si sahihi ila mwisho wa siku mahakama ndiyo itatafsiri ni bodi ipi sahihi, na uongozi upi sahihi,” amesema.



Chanzo: Dewji Blog na GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo