Habari Mpya tena za Ujenzi wa Barabara ya lami Makete Njombe (AUDIO)

Hatua za ujenzi wa barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha lami zimeendelea kutekelezwa, baada ya uongozi wa kijiji cha Tandala Wilayani Makete kuutangazia umma hatua wanazotakiwa kuzifanya kuanzia Jumatatu Ijayo ili kupisha ujenzi wa barabara hiyo

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Afisa Mtendaji wa kijiji Cha Tandala Bw. Bruno Mhiche imewataka wananchi wote waliojenga ndani ya mita 22.5 toka katikati ya barabara ya Makete Njombe kufika katika ofisi za Kijiji hicho kwa lengo la kupokea taarifa rasmi kutoka TANROADS za kupisha ujenzi huo

Mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Andowise Memba akizungumzia hatua hiyo, amewataka wananchi hasa wahusika kutoa ushirikiano kwa serikali kwa lengo la kupewa utaratibu wa kupisha ujenzi huo kama ambavyo serikali imetangaza


Katika kipindi cha mwaka huu wa fedha 2016/2017 serikali kupitia wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano tayari imetangaza Ujenzi wa barabara ya Makete Njombe kwa kiwango cha lami 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo