Maamuzi ya wananchi wa Tandala Makete baada ya Kukosa maji Muda Mrefu

Katika kuendeleza juhudi za kutatua tatizo la maji katika Kijiji cha Tandala wilayani Makete Mkoani Njombe, Mkutano wa dharura wa kijiji hicho umeunda timu maalum kwa ajili ya kufanikisha kuondokana na tatizo la maji kijijini hapo

Timu hiyo iliyoundwa imehusisha wajumbe wawili kutoka Kila kitongoji cha Kijiji hicho, na hali hiyo inafuatia majadiliano ya pamoja na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo ukiwa na ajenda moja ya kujadili kero ya maji

Mwenyekiti wa kijiji hicho Andowise Memba akaanza kwa kuufungua mkutano huo na kueleza lengo lake


Diwani wa kata hiyo Mh Egnatio Mtawa amewataka wananchi hao kutambua kuwa suala la ukosefu wa maji linamhusu kila mtu, na sehemu nzuri ya kusemea ni katika mikutano ya hadhara


Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wakatoa mapendekezo yao namna ya kuondokana na kero hiyo ya maji kabla ya kupatiwa elimu ya kuupata uongozi wa kushughulikia maji kutoka kwa mtaalamu wa Idara ya Maji kutoka halmashauri ya wilaya ya Makete


Katika hatua nyingine akizungumza katika Mkutano huo Diwani wa kata hiyo Mh Mtawa amewaambia wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji na kusema hatakuwa na huruma na wale wanaochezea vyanzo vya maji vilivyopo katika kata yake


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo