Imeelezwa kuwa baada ya muda si mrefu huwenda halmashauri
ya wilaya ya Makete mkoani Njombe ikakumbwa na uhaba wa watumishi kutokana na
zoezi la uhakiki wa watumishi linaloendelea kufanywa na serikali
Akijibu hoja ya Mh Ilomo iliyoibuliwa katika baraza la
madiwani wa halmashauri hiyo kuhusu upotevu wa mapato ya kata ya Kigala
kutokana na kukosekana watendaji Afisa utumishi na Utawala wilaya ya Makete Bw.
Nicodemus Tindwa amesema kutokana na zoezi la uhakiki wa vyeti linaloendelea
sasa, lemepelekea serikali kusimamisha ajira zote hivyo wapo pia watumishi
watakaokosa sifa kutokana na zoezi hilo ambalo bado linaendelea
Amesema anatambua ukosefu wa watendeji wa vijiji vya
Kinyika na Ndapo lakini hana uwezo wa kuwapeleka watumishi wapya kwa sasa mpaka
hapo serikali itakapotoa kibali cha ajira za watumishi
Wakati huo huo halmashauri kupitia baraza hilo la
madiwani imetolea ufafanuzi wa matumizi ya sheria ya mazingira inayokataza
kufanyika shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, kingo za mito,
mabwawa, maziwa na bahari ndani ya mita 60, ambapo afisa mazingira Raphael
Kalongola amesema mpaka sasa mita 60 zipo palepale ingawa wapo kwenye hatua za
kumuandikia barua waziri wa mazingira kuomba utekelezaji wa sheria hiyo kwa
Makete ubadilishwe
Wakati huu ambapo yanasubiriwa majibu ya waziri Kuhusu
ombi hilo sheria ya sasa ya mazingira bado ipo palepale na inaendelea kutukima
na kutekelezwa kama ilivyo. sikiliza sauti hapo chini