Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe baada
ya kujigeuza kama kamati, wameridhia kuwafukuza kazi watumishi wa halmashauri
hiyo kutokana na makosa mbalimbali waliyoyatenda
Akitangaza uamuzi huo katika baraza la Madiwani hapo jana, Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Mh. Egnatio Mtawa amesema jumla ya watumishi 13 wamejadiliwa,
9 kati yao wamefukuzwa kazi huku wengine wakichukuliwa hatua nyinginezo ikiwemo
kushushwa cheo
Hata hivyo kupitia baraza hilo wapo watumishi wengine waliowajibishwa kwa
kuondolewa majukumu yao ili kupisha uchunguzi kutokana na Mchakato wa uvunaji
wa msitu wa Iwawa na Nungu kufuatia
kasoro zilizojitokeza huku Mkurugenzi akiagizwa kuunda timu ya uchunguzi
wa suala hilo ambayo itatakiwa kuleta taarifa yake rasmi baada ya miezi miwili
kuanzia oktoba 28
Aidha madiwani hao pia wamewathibitisha kazini jumla ya watumishi na
msisitizo kutolewa kwao kuwa wafanye kazi zao kama serikali ya awamu ya 5
inavyotaka
sikiliza sauti hizi hapa chini:-