Angalia Kilichotokea Mpaka Rais Magufuli akaomba kutembea Kwa Miguu Nchini Kenya

Katika hali ambayo sio ya kawaida kwa kiongozi kama rais wa nchi, Rais John Magufuli ambaye yupo nchini Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili amekutana na foleni wakati akielekea katika eneo ambalo alizikwa Rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, aliuambia mtandao wa Star wa Kenya kuwa Rais Magufuli alikutana na foleni hiyo wakati akitokea katika hoteli ya Intercontinental na kuelekea eneo la alilozikwa Jomo Kenyatta na baada ya kuona kuna foleni kubwa alitaka kutembea ili aweze kufika eneo ambalo anataka kwenda kuliona.
Aidha baada ya kutoka eneo hilo alikuta tayari maafisa wa usalama wameshaweka magari mengine pembeni ya barabara ya Uhuru na hivyo aliweza kupita kwa urahisi kuelekea ikulu kukutana na mwenyeji wake, Rais Uhuru Kenyatta.
Baada ya kuwasili ikulu JPM alionana na Rais Kenyatta na kufanya mazungumzo kisha kulihutubia taifa la Kenya kuhusu mahusiano ya Kenya na Tanzania na mipango ambayo wameiweka baada ya kufanya mazungumzo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo