Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakipima eneo la tukio la ajali iliyohusisha gari la Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa Tamisemi Suleiman Jafo katika kijiji Katela kata ya Kiwira Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.(Picha na Keneth Ngelesi)
;;;;;;;
Naibu Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jafo amepata ajali eneo la Katela Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya.
Ajali hiyo imehusisha gari dogo aina ya Corola iliyokuwa ikotokea Mbeya kwenda Rungwe na Naibu Waziri Selemani Jafo alikuwa akitokea Tukuyu kikazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema katika gari Waziri walikuwa watatu, Waziri Jafo mwenyewe Katibu wake na Dereva na wote walitoka salama katika ajali hiyo.
Alisema baada ya kupata ajali hiyo walipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi kama wameumia kwa ndani au laa! Lakin bahati nzuri Daktari aliyewafanyia uchunguzi alisema hakuumia popote ni wazima.
Alisema baada ya hapo Waziri na watu waliendelea na safari yao kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kuwahi vikao vya Bunge


