Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali ombi la dhamana kwa washitakiwa sita akiwemo aliyekuwa mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya Taifa NIDA Bwana Dickson Maimu wanaotuhumiwa kwa makosa ya kuisababishia hasara serikali ya zaidi ya shilingi bilioni 1.2.
Maamuzi hayo ya mahakama kuu yamesomwa na msajili wa mahakama kuu Projestus Kayoza ambaye amesema mahakama imefikia maamuzi hayo baada kubaini mapungufu katika hati ya kiapo, iliyowasilishwa mahakamani hapo kwa ajili ya maombi ya dhamana,
Ameiambia mahakama kuwa maombi ya sasa ya dhamana kwa watuhumiwa hao sita yamebainika kuwa na mapungufu kadhaa ya kisheria ambapo pia yaliombwa katika kiapo ambacho kimebainika kuwa na mapungufu, na hivyo kuamua kutupilia mbali ombi la dhamana kwa vigogo hao waliokuwa wakishikilia nafasi za juu za uongozi katika mamlaka ya vitambulisho vya Taifa.
Awali akisoma maamuzi kuhusu mabishano ya kisheria kuhusu kasoro zilizopo kwenye kiapo cha maombi ya dhamana kilichowasilishwa na upande wa utetezi wa watuhumiwa na kupigwa vikali na mawakili wasomi wa serikali wakiongozwa na Fredrick Mayanda, msajili huyo wa mahakama amesema miongoni mwa mapungu yaliyobainika katika kiapo hicho ni ukosefu wa chanzo cha taarifa ambazo ziliwasilishwa na wakili wa watuhumiwa hao Michael Ngaro.
Washitakiwa hao wanaoshitakiwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 1.Ambao bado wanaendelea kusota mahabusu kwa kukosa dhamana ni pamoja na aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo, Bw Dickson Maimu.
