skip to main |
skip to sidebar
Daktari aliyewaambukiza UKIMWI wagonjwa 200 atupwa jela miaka 25
Daktari aliyewaambukiza wagonjwa 200 virusi vya ukimwi nchini Cambodia amehukumiwa jela.Daktari huyo bandia alipatikana na hatia ya kuwaambukiza takriban watu 200 virusi vya ugonjwa wa Ukimwi amehukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa makosa yake.
Baadhi ya wahasiriwa wa makosa hayo wamekwisha fariki dunia.
Yem Chrin alikuwa akitumia sindano zilizokuwa zimekwisha tumika kuwatibu wenyeji wa kijiji cha Roka bila ya kujua alickuwa akisambaza Virusi vya Ukimwi.Awali Chrin alikuwa ameshtakiwa kwa mauaji lakini upande wa mashtaka ukabadilisha shtaka na kuwa kuua bila ya kukusudia.
Kesi hiyo imefichua uhaba wa madaktari na ugumu ulioko kwa raia kupata huduma za afya katika maeneo mengi ya vijijini nchini Cambodia.
Utafiti umebaini kuwa zahanati nyingi katika maeneo ya vijijini huendeshwa na madakatari bandia ambao hawajahitimu kuwatibu wagonjwa.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi