Basi lagonga Lori huko Shinyanga na kuua watu

Watu wanne wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya JM Luxury Coach lenye namba za usajili T.159 DYZ  kugonga lori lenye namba za usajili T.218 ABY aina ya TATA katika barabara ya Shinyanga kwenda Mwanza katika eneo la njia panda ya kwenda wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.


Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ajali hiyo imetokea Jana majira ya saa mbili asubuhi wakati basi hilo likitoka jijini Mwanza kwenda Dar es salaam kugonga lori lililokuwa linakata kona kwenda wilayani Kishapu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi lenye namba T.159 DYZ aina ya Yutong mali ya kampuni ya JM Luxury Coach likiendeshwa na Sarehe Kassim(46) mkazi wa Dar es salaam.

 “Chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa basi likitaka kulipita lori ambalo lilikuwa likikata kona kuelekea wilaya ya Kishapu na kuligonga upande wa kulia na kusababisha vifo vya watu wanne ,wote wanaume waliokuwa ndani ya lori akiwemo dereva wa lori na wote hajatambulika miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga,na kujeruhi watu wanne waliokuwa ndani ya basi”,ameongeza Kamanda Muliro.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo