ZAIDI
ya wavuvi tisa waliokuwa wakifanya shughuli zao za uvuvi ndani ya mto
Kagera wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa nyakati
tofauti.
Akisoma
taarifa ya Wilaya kwa Waziri wa mambo ya ndani ya nchini Lameck Mwigulu
Nchema,Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kanali mstaafu Shaabani Lissu alisema
kuwa wavuvi hao wanatokea katika mialo ya Rubwela,Kanyika,katwe na Ruko
katika ziwa ngoma.
Alisema
matukio hayo ya vifo vya utata yameanza kutokea kuanzia mwezi wa pili
mwaka huu wakati wavuvi hao wanapoenda kuvua ndani ya mto Kagera
unaotenganisha nchi ya Rwanda na Tanzania.
"Mara
nyingi wavuvi wakienda kuvua ndani ya Mto Kagera huwa hawarudi,huwa
wanatekwa na kuuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni
askari wa nchi jirani ya Rwanda"Alisema Mkuu huyo wa Wilaya
Alisema
hivi karibuni wavuvi wawili walienda kuvua ndani ya mto Kagera na mmoja
aitwaye Emanuel Kahonda alipigwa risasi na kufariki dunia huku mwenzake
Yoha Misago akinusurika katika tukio hilo na kukimbia na kwenda kutoa
taarifa kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
"Mhe.Waziri
ni juzi tu kuna mvuvi alipigwa risasi ndani ya mto Kagera hata msiba
kwake bado upo, mwenzake aliyeshuhudia na kufanikiwa kuwatoroka wauaji
hao yeye kunusurika ndiyo alikuja kutoa taarifa ofisini kwangu"alisema
Naye
mwenyekiti wa mwalo wa Kitwe Ustadhi Hakimu alimthibitishia Waziri kuwa
wavuvi wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kuuwawa kikatili na askari wa
nchi jirani ya Rwanda.
"Hapa
kijijini kuna wajane wengi,waume zao walikuwa wakienda kuvua samaki
ndani ya mto Kagera hawarudi,wanadai tunavua samaki kwenye maji yaliyopo
nchi mwao,na mto kagera wameufanya wao peke yao,Tunaomba utusaidie
Mhe.Waziri hili tatizo liishe
Upande
wa kule kwao kuna misitu sana na huwa wanajificha humo,yaani wakikuona
tu wala hawakusemeshi wanakupiga risasi tu humo humo majini,na maiti
zimekuwa zikipotelea mtoni humo humo"alisema Mwenyekiti huyo.
Naye
waziri wa mambo ya ndani ya nchini Mwigulu Nchemba aliiagiza kamati ya
ulinzi na usalama ya Wilaya ya Kyerwa kukutana na viongozi wa mialo ili
wapate taarifa rasmi ya chanzo cha matukio hayo na kuipatia wizara ili
waweze kutoa tamko rasmi juu ya mauaji hayo ya wavuvi.
"Hali
hii imenistua sana,hatuwezi kuruhusu watanzania wenzetu wawe wanauwawa
kikatili kiasi hiki,nikipata taarifa rasmi nitafuatilia jambo hili hata
kwa kuwasiliana na wenzetu ili nijue kama ni msimamo wa serekali yao au
ni uhalifu"alisema Nchemba.