Rais
Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete leo ametoa tamko la Timu ya Waangalizi wa
Uchaguzi wa Jumuiya ya Madola la Uchaguzi Mkuu wa Zambia uliofanyika
tarehe 11 Agosti, 2016 kuchagua Rais, Wabunge, Mameya, Madiwani na Kura
ya Maoni ya Katiba.
Rais
Mstaafu Kikwete yuko nchini Zambia kufuatia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Madola kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu hiyo yenye waangalizi wa
kimataifa 17 kutoka nchi za Jumuiya ya Madola.
Kwa
mujibu wa tamko hilo, Jumuiya ya Madola imejiridhisha kuwa zoezi la
upigaji kura, usimamizi wa kura na uhesabuji kura vituoni kwa ajili ya
umeendeshwa kwa uwazi na kwa kuzingatia kanuni bora za uendeshaji wa
chaguzi.
Tamko linasema, dosari na hitilafu zilizojitokeza hazikuwa kubwa kiasi cha kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu huo.
Amewapongeza
wananchi wa Zambia kwa kufanikisha zoezi la uchaguzi kwa amani na
kutumia haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Amewasihi
viongozi wa kisiasa wa Zambia, wagombea na vyama vya siasa kuheshimu
maamuzi wa wananchi na pale inapojitokeza upande wowote kutoridhika na
matokeo, zitumike njia za amani na kisheria za kutafuta ufumbuzi.