Watu 3 wanashikiliwa na polisi Morogoro kwa tuhuma za kusafirisha bangi kwenda DSM

Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha kilo 75 za madawa ya kulevya aina ya Bangi yakiwa yanasafirishwa kutoka mkoani Morogoro kuelekea jijini Dar es Salaam ambayo yalifungwa katika mifuko na maboksi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao katika njia panda ya kuelekea chuo kikuu cha Mzumbe wakiwa wamepakia mizigo kwenye pikipiki maarufu (bodaboda) ambapo baada ya kukamatwa walifanyiwa upekuzi na kukutwa na madawa hayo.

Aidha katika tukio jingine kamanda Matei amesema jeshi hilo limefanikiwa kuipata silaha ambayo ilikuwa imetelekezwa na mtu asiyefahamika katika mtaa wa Bong’ola manispaa ya Morogoro baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema ambapo askari walifika na kuichukua silaha hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo