Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akiongozana na Kamanda Simon Sirro wakikagua gari ambapo askari waliouawa walikuwemo
Watu 13 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamewaua polisi wanne
katika uvamizi wa Benki ya CRDB eneo la Mbande kata ya Mbagala wilaya ya
Temeke jijini Dar es Salaam, na kutoweka na kusikojulikana.
Akizungumza na East Africa radio, leo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Dar es Salaam, Simon Sirro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa limetokea jana majira ya saa moja na nusu jioni wakati
askari hao wakibadilishana lindo na ndipo walivamiwa na majambazi hao.
Kamanda Sirro amesema kuwa licha ya kufanya tukio hilo pia majambazi hao walivamia kituo cha polisi cha Mbande na kisha kuchukua sare ya polisi na kukimbia nazo ambapo amesema jeshi la polisi linaendelea kuwasaka wahusika wa tukio hilo.
Aidha Kamanda huyo wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ametumia Fursa huyo kuwataka Wakazi wa Dar es Salaam kuwa watulivu na kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa kufanikisha kuwakamata watu hao ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Kuhusu Majina ya Polisi waliouwa Kamanda Sirro amesema wamekwisha tambulika lakini hawezi kuyaweka majina yao kwa sababu za kiusalama na kuongeza ana imani watuhumiwa hao watakamatwa wakati wowote kuanzia hii leo.
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba aliyefika eneo la tukio usiku huo huo amesema askari hao walivamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha katika eneo hilo na kuwaua askari hao waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo.
Amesema mbali na vifo hivyo, pia raia wawili wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu.

Waziri Nchemba amesema mbali na kulaani tukio hilo amewataka wahusika kujisalimisha na wananchi kutoa ushirikiano.
“Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu”. Amesema Waziri Mwigulu