MKE
wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Elisaria Msuya (41) amefikishwa
mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya dada wa wa bilionea huyo, Aneth
Msuya.
Mshtakiwa
huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana jijini Dar
es Salaam na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo
mbele ya Hakimu Mkazi, Margareth Bankika.
Akisoma
mashtaka hayo, Lukondo alidai mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa maeneo
ya Sakina kwa Iddi, jijini Arusha anadaiwa Mei 25, mwaka huu katika
maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam alimuua Aneth Elisaria
Msuya.
Mshtakiwa
hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa
kusikiliza kesi za mauaji, mbapo Jamhuri ilidai upelelezi haujakamilika
na kuomba kesi hiyo ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Bankika, alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alirudishwa rumande.
Habari
zilizopatikana baada ya tukio hilo zilidai kwamba, marehemu Aneth
aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Mei 25,
mwaka huu Dar es Salaam.
Mauaji
hayo yalitokea nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni ambako
inaelezwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.
