Watu wasiopungua 12 wamefariki baada ya kunywa pombe haramu katika mkoa wa Bihar nchini India.
Mkuu wa polisi ameeleza kuwa waliofariki walikunywa pombe hiyo Jumatatu jioni na walianza kuumwa siku moja baadaye.
Watu wengine watano pia wanatibiwa katika hospitali moja baada ya kutumia kinywaji hicho.
Vifo kutokana na unywaji wa pombe haramu hutokea mara kwa mara nchini India kwa sababu watu maskini hawawezi kununua pombe zilizopewa kibali cha kuuzwa.
Mara nyingi pombe haramu huchanganyiwa kemikali na dawa za kuua wadudu ili kuongeza ukali wake.

BBC