Katika chuo hicho bweni linatumika kama darasa na wakati huo huo likitumika kama ofisi na vyoo vya wasichana na wavulana huku vyoo hivyo vikiwa vichafu na vibovu hali inayohatarisha afya za wanafunzi hivyo mkuu wa wilaya Tunduru Bw.Juma Homera ametangaza kukifunga chuo hicho huku saini ya barua ya kukiruhusu kuendesha shughuli zake wilayani Tunduru ikidaiwa kughushiwa.
Kaimu Mkuu wa Chuo hicho kinachodaiwa hakijasajiliwa huku wanafunzi wakitozwa ada ya shilingi laki saba kwa mwaka bw.Hassan Muya mwenye elimu ya cheti anasema kuwa hatua ya kukifungia chuo hicho anaichukulia kawaida.
Kwa upande wao wanafunzi wa chuo hicho ambao wanalala chini huku wengine wakilala kwenye meza ndani ya darasa akiwemo Shukrani Exaveri kutoka wilayani Biharamulo mkoani Kagera wanaiomba serikali kuvifungia vyuo vingine vinavyoendeshwa kimagumashi ili wengine wasipate hasara kama waliyoipata wao huku wakiiomba serikali kuhakkikisha wanapata vyuo vyenye sifa kwa kuwa wanazo sifa.