Kijana huyu amekutwa Asubuhi ya leo amejinyonga maeneo ya Mlimani City Opposite na Mawasiliano Tower.
Kwamujibu wa Mashuhuda kijana huyu amekutwa amejinyonga na Kipande cha
shuka na chini yake kulikuwa na begi lenye nguo yani inaonyesha kuwa
huyu Kijana alikuwa katoka safarini pia marehemu amekutwa na ana jeraha
mkono wa Kushoto na damu katika fulana maeneo ya kifuani.
Mashuhuda wanasema kuwa inawezekana kuwa huyu kijana alipigwa na watu
kisha alipo fariki wakamtundika Mtini ili aonekanike kama kajiyonyanga
mwenyewe maana amekutwa kaumia mkononi pia ana damu kifuani kwamujibu wa
mashuhuda wanasema mtu anayejinyonga huwa lazima akutwe kajinyea au
kajikojolea marehemu amekutwa yuko safi kabisa, pia Mtu aliyejinyonga
huwa hatoki Damu kwahiyo inawezekana kuwa alipigwa kisha akatundikwa mtini
ili aonekane kama kajinyonga mwenyewe.. M/mungu ailaze roho ya marehemu
mahala pema peponi.. Amin