Rais
wa awamu ya pili wa Zanzibar na Mwenyekitiwa Baraza la Mapinduzi
(1972-1984), Mzee Aboud Jumbe Mwinyi amefariki dunia jana baada ya kuugua
kwa muda mrefu.
Mzee Aboud Jumbe amefikwa na mauti hayo nyumbani kwake Kigamboni, Jijini Dar es salaam. Rais wa Jamhuri wa Muungano amemtumia Salaam za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa msiba huu mzito