Ikiwa ni siku nne tangu gazeti la Mwananchi ilipoandika taarifa juu ya kupotea kwa binti Neema Herman (15), mkazi wa Kaloleni, walezi wake wamesema wameshampata mtoto huyo katika eneo la Ngusero, Arusha alikofichwa ndani na kijana ambaye ni dereva bodaboda.
Baba mdogo wa binti huyo, Bryson Masawe alisema alipigiwa simu na wasamaria wema siku ya alhamisi Agosti 4, ambao walimuelekeza mahali binti huyo walipomuona.
“Tulivyofika majira ya saa sita mchana, tulimkuta anakunywa chai na kiporo ila mwanaume hatumkuta ndani,” alisema.
Aliongeza kuwa kijana aliyemuweka Neema ndani kwake ni dereva bodaboda, mkazi wa Ngasero, Arusha ila hawakufanikiwa kumkamata na kwamba anaendelea kutafutwa.
Taratibu za kumpeleka hospitali kwa ajili ya vipimo zilifanyika na kuambiwa inatakiwa warudi tena baada ya mwezi mmoja kwa ajili ya kufanya vipimo tena ikiwamo mimba.
Aidha baada ya kutoka hospitali, Masawe alisema walielekea shuleni ambako Neema alitakiwa kutoa maelezo kutokana na tukio lililotokea.
Alitoa wito kwa wazazi na walezi wote kufuatilia mienendo ya watoto wao na mahudhurio na maendeleo shuleni ili kuwaweka karibu zaidi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kaloleni Magharibi mkoani humo, Hassan Sharifu alisema baada ya mtotro kupatikana familia ilimpeleka mtoto huyo kwake kuripoti na baadaye walimpeleka hospitali kwa vipimo zaidi vya kiafya.
Mwalimu wake wa darasa, Monica Mwanga alisema Neema alifikishwa shuleni na kutoa maelezo na kwamba kwa sasa wanamsubiri baba mzazi ambaye ni dereva wa lori kwa sasa yupo safarini.
“Maamuzi yatatolewa baada ya mzazi wake kufika shuleni na nitoe ushauri kwa wazazi wasiwaachie walimu mzigo wa kuwafatilia watoto bali tushirikiane kuhakikisha watoto wana maadili mazuri,” alifafanua Mwanga.