Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilianoa prof.MAKAME MBARAWA
amemsimamisha kazi kaimu Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege Tanzania
ATCL Captain Jonson Mfinanga na Mkurugenzi wa uendeshaji Captain Sadick
Muze kwa kosa la kuchagua rubani mmoja asiye na sifa kati ya marubani
watano wanaotarajia kuondoka hapo kesho kwenda nchini Canada kwa ajili
ya mafunzo ya kurusha ndege mpya zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati
ya mwezi Septemba.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoni Mbeya Pro.Mbarawa amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya shirika la ndege Tanzania ATCL alitoa maelekezo kwa kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo kuwachagua marubani watano wenye sifa ili waende nchini Canada kwa ajili ya mafunzo ya kurusha ndege hizo pindi zitakapo wasili jambo ambalo amesema miongoni mwa marubani hao watano waliochaguliwa mmoja hajatimiza vigezo hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.
Aidha waziri huyo amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhahakikisha kila mtumishi wa umma anatekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo haitasita kumchukulia hatua kali zakinidhamu.
Chanzo: ITV