Polisi inawashikilia baba mzazi na mwanaye kwa tuhuma za
kuozesha mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14, baada ya kukatishwa masomo katika Shule ya Msingi Chembeli wilayani Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Jumanne Muliro aliwataja wanaoshikiliwa kuhusiana na matukio matatu ya kuwaoza wanafunzi yaliyotokea mwezi mmoja uliopita kuwa, ni baba mzazi wa mtoto huyo, Hamisi Makenzi na bwana harusi, Dotto Ngassa (19).
Kwa Julai pekee, wanafunzi watatu wenye umri kati ya miaka 14 hadi 16 waliokuwa wakisoma shule za msingi na sekondari wilayani hapa wamekatishwa masomo na kuozeshwa.
Wafunzi hao waliokuwa wakisoma Chembeli na Sekondari ya Usanda, waliozeshwa baada ya wazazi wao kupokea mahari ikiwa ni mwendelezo wa mila na desturi inayowachukulia watoto wa kike kama kitega uchumi.