Akizungumzia
tukio hilo, kaka wa Suzana, Dabirian Kinyolo alisema jana kuwa mdogo
wake alirudi nyumbani usiku akitokea kilabuni kunywa pombe, alifika na
kuwasha kibatari karibu na kitanda chake jambo lililosababisha moto kushika chandarua.
Kinyolo alisema katika tukio hilo wajukuu wawili wa Suzana
ambao ni Ratifa Siyajali (4) na Rehema Siyajali (2), walinusurika baada ya kukimbia kutoka ndani walipoona moto unazidi.
ambao ni Ratifa Siyajali (4) na Rehema Siyajali (2), walinusurika baada ya kukimbia kutoka ndani walipoona moto unazidi.
“Kwa sababu Suzana alikuwa amelewa sana, alishindwa kukimbia hivyo kuteketea akiwa ndani ya nyumba,” alisema Kinyolo.