Mama anayedaiwa kuchoma maduka matatu, nyumba yake ya kuishi Arusha ajinyongea mahabusu

August 21 2016 ziliripotiwa habari za mama mmoja anayejulikana kwa jina la Victoria Edward Wenga kuchoma moto maduka matatu na nyumba yake ya kuishi katika kata ya Lemara Arusha.

Chanzo cha  mama huyo kuchoma moto ilidaiwa ni ugomvi uliokuwepo kwenye familia kati ya mama huyo na mume wake anayejulikana kwa jina la Edward Wenga. 

Habari nilizozipokea muda si mrefu Mama zinasema kwamba mama huyo amejinyonga kwa kutumia nguo yake na kufariki dunia.

Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amesema alijinyonga akiwa kituo cha polisi kama mahabusu ambapo polisi walipata taarifa baada ya mahabausu wenzake kupiga kelele.

Chanzo: Millard Ayo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo