Mkurugenzi wa Halmashauri Atiwa mbaroni akidaiwa kuiba

Vita dhidi ya ufisadi inazidi kupamba moto mkoani Kilimanjaro baada ya Polisi kumtia mbaroni mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Rashid Kitambulilo.

Kukamatwa kwa Kitambulilo ambaye ni miongoni mwa wakurugenzi 120 walioachwa na Rais John Magufuli kumekuja wakati Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ikimchunguza kutokana na tuhuma za rushwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kukamatwa kwa Kitambulilo kwa  tuhuma za wizi akiwa mtumishi wa umma.

Kwa mujibu wa Mutafungwa, Kitambulo alikamatwa Jumapili iliyopita na kuhojiwa kisha kuachiwa kwa dhamana jana.

Hata hivyo, kamanda huyo alikataa kuzungumzia kwa undani kuhusu tuhuma zinazochunguzwa, lakini taarifa za uhakika zilieleza ni ubadhirifu wa Sh9 milioni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Uchunguzi huo umekuja wakati Takukuru ikiendelea kuwahoji watumishi 11 wa halmashauri hiyo kuhusiana na ubadhirifu wa zaidi ya Sh110 milioni za uchaguzi huo.

Kamanda wa Takukuru mkoani humo, Alex Kuhanda alilithibitisha kuhusiana na uchunguzi huo, lakini alikataa kuingia kwa undani akisema sheria haimruhusu kufanya hivyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo