Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akitembelea Kituo kikuu Ubungo cha Mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani, leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na sehemu ya
Wananchi waliokuwepo kwenye Kituo Kikuu cha Ubungo, Jijini Dar es salaam
leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akiwasalimia wananchi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemtaka Mkurugenzi wa jiji
kuanza mchakato wa kuhamisha kituo kikuu cha mabasi ya mkoani cha
ubungo kuhamia Mbezi mwisho
Makonda
ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo hicho leo, amesema kituo
hicho kimeelemewa na idadi ya kubwa ya wasafiri huku miundombinu
haiendani na utoaji wa huduma kwa wasafiri wanaotumia kituo hicho.
Makonda
amesema kuwa baada ya kituo hicho kuhama panatakiwa kufanyika
uwekezaji wa soko kubwa ili kupunguza msongamano wa watu katika soko
la Kariakoo.
Aidha
Makonda amesema kuwa uamuzi huo umetokana na kuonekana kwa kituo hicho
kuwa kidogo na kushindwa kutoa huduma ya usafirishaji ya abiria
wanaoingia na kutoka katika mikoa mbalimbali.
Makonda
ameutaka uongozi wa kituo hicho kufunga taa maeneo yote kutokana na
kutawala kwa giza nyakati za usiku,ambapo ni hatari kwa usalama wa
abiria wanaoshuka nyakati hizo.
RC
Makonda pia amepiga marufuku kukamata magari kwa kigezo cha maegesho,
wakati hakuna alama zinazoonyesha sehemu ya kuegesha magari.