Wanafunzi wakatisha masomo kutafuta fedha za matibabu mitaani

Wanafunzi wawili wa darasa la saba wanaosoma katika Shule ya Msingi Rwemishesha Bukoba Vijijini, Diana na Dorine Baina wamelazimika kukatisha masomo kuchagisha fedha mtaani kwa ajili ya kumtoa baba yao aliyelazwa katika hospitali ya Kagondo mkoani Kagera.

Mgonjwa huyo, Baina Baltazar amelazwa katika hospitali hiyo tangu Februari mwaka huu baada ya kupata ajali ya gari katika mguu wake wa kulia na anadaiwa Sh571, 500 ili aweze kuruhusiwa hospitalini hapo.

Hatua hiyo imewalazimu watoto wake kwa kibali cha katibu tawala wilaya ya Bukoba kuingia mtaani kuanzia Mei 18 hadi Julai 18, mwaka huu kuomba msaada wa fedha kumtoa baba hospitali.

Baltazar alifanyiwa upasuaji mara nne katika mguu wake baada ya kugongwa na gari, hivyo hana budi kuwatumia watoto wake wamsaidie kutafuta fedha aweze kutoka hospitalini.

“Nimezuiwa kuondoka baada ya kufanyiwa upasuaji mara nne mpaka nitakapolipa gharama za matibabu,” alisema Baltazar.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo