Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ameagiza kusakwa kwa
wazazi wa wanafunzi 12 wa shule za msingi wilayani Bahi baada ya watoto
wao kupata ujauzito.
Akizungumza baada ya kumwapisha Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius
Ndejembi, Rugimbana aliwataka wakuu wa wilaya kupambana na tatizo la
njaa katika wilaya zao ambalo linachangia wanafunzi wa kike kupata ujauzito.
"Bado kuna upungufu mkubwa wa chakula katika baadhi ya maeneo na mahali
panapoathirika zaidi ni kwenye elimu hasa kwa wanafunzi wa kike" alisema.
Alisema mwaka huu Wilaya ya Bahi ina wanafunzi 12 wa Shule ya Msingi
ambao wana ujauzito na amewaagiza watendaji wa wilaya hiyo kuwatafuta
wazazi wao.
Alisema wazazi wanawajibika katika malezi ya watoto wao na ndiyo maana
ameagiza wasakwe.