Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kesi wakati
alipofika kijijini hapo kusikiliza kero za wananchi ikiwemo baada ya wao
kutangaza kugomea shughuli za maendeleo kwa madai ya kutoridhishwa na
mwenendo wa shauri la kuuawa mtoto mmoja kijijini hapo na watuhumiwa wa
mauaji hayo kupewa dhamana
Mh
Kesi amesema anaungana na wananchi hao kuwapa pole kwa msiba huo
uliowapata na kusema hoja zote zilizotolewa na wananchi katika mkutano
huo amezichukua na kuahidi kwenda kuzifanyia kazi na wananchi kuona
majibu kwa kuwa ziko hoja ambazo zipo ndani ya uwezo wake na nyingine
zilizopo kwa upande wa mahakama watashirikiana na wataalamu wakiwemo
wanasheria kuzitatua kisheria
Pia
mkuu huyo amelaani mauaji hayo na kusema si vizuri mtu yeyote
kujichukulia sheria mikononi na kusababisha kifo cha mwananchi yeyote
Sikiliza sauti hizi