Ofisa Habari wa klabu ya Simba Bw. Haji Manara Apoteza Uwezo wa Kuona

Kunastori inazidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidai Ofisa Habari wa klabu ya Simba Bw. Haji Manara amepoteza uwezo wa kuona. 

Taarifa zinadai awali jicho lake moja lilipoteza kabisa uwezo wa kuona na akapanga kukutana na mtaamu wa macho ili kupata ufumbuzi wa tatizo linalomkabili.

Taarifa nyingine zimetoka usiku huu (Julai 5) kwamba jicho ambalo lilikuwa linauwezo wa kuona, nalo limepoteza uwezo huo na kumfanya Manara asione kabisa kwa macho yake mawili.

Mdau wa Michezo Shaffih Dauda naendelea kutafuta ukweli wa taarifa hii ikiwa ni pamoja na kumpigia simu Manara ili athibitishe kama taarifa hizi ni za kweli au ni uvumi wa mitandaoni. Tutaendelea kukujuza kadiri tutakavyopata taarifa rasmi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo