Rushwa Mkoa Wa Njombe Inawashikilia Watumishi Wake Wawili Wa Wilaya Ya Makete Kwa Tuhuma Za Kujihusisha Na Ufisadi Na Kuomba Rushwa Ya Shilingi Laki Sita Kwa Mwananchi Jina Lake Limehifadhiwa Kwa Usalama Wake Ambaye Alikuwa Anakabiliwa Na Tuhuma Za Kugushi Vyeti Vya Ajira Wilayani Humo.
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ofisini Kwake Kamanda Wa Takukuru Mkoa Wa Njombe Charles Nakembetwa Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa Ni Pamoja Na Mwanasheria Wa Taasisi Ya Takukuru Wilaya Ya Makete Frednand Nsakuzi Pamoja Na Mlinzi Wa Ofisi Ya Takukuru Makete Julius Hasani Wote Watumishi Wa Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa Wilayani Makete.

Kamanda Nakembetwa Amesema Watuhumiwa Hao Kwa Pamoja Waliomba Kiasi Hicho Cha Fedha Shilingi Laki Sita Kwa Mwananchi Ambaye Jina Lake Limehifadhiwa Katika Tukio Lililotokea June 28 Mwaka Huu Majira Ya Saa Moja Na Saa Mbili Usiku Ambapo Waliomba Rushwa Kwa Mwananchi Huyo Aliyekuwa Anatuhumiwa Kugushi Vyeti Vya Ajira.
Charles Nakembetwa Amemwambia mwandishi wetu Kuwa Watuhumiwa Hao Walifanikiwa Kupokea Fedha Ya Awali Shilingi Laki Moja Ambapo Baada Ya Takukuru Mkoa Wa Njombe Kupata Taarifa Hizo Walifanikiwa Kuweka mtego Na Kuwakamata Wahusika Wakiwa Wanachukua Fedha Hizo Kinyume Na Kifungu Cha 15 Cha Sheria Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa Namba 11 Ya Mwaka 2007.
Amesema Watuhumiwa Hao Walitenda Kosa Hilo Kinyume Na Sheria Ya Makosa Ya Jinai Na Kosa La Kutoa Siri Za Ofisi Wakiwa Watumishi Wa Umma Na Kwamba Taratibu Za Kuwasimamisha Kazi Zinaendelea Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwafikisha Mahakamani Kujibu Tuhuma Zinazowakabili Mara Baada Ya Uchunguzi Kukamilika.
Aidha Takukuru Mkoa Wa Njombe Imewashukuru Baadhi Ya Wananchi Wanaoendelea Kuonesha Ushirikiano Huo Wa Kutoa Taarifa Za Vitendo Vya Rushwa Vinavyoendelea Kufanyika Miongoni Mwa Viongozi Wa Serikali Na Watu Binafsi Kwani Vitendo Hivyo Vitatokomezwa Endapo Wananchi Wataonesha Mshikamano Huo.