Mkuu mpya wa wilaya ya Makete atema cheche, "No siasa hapa ni kazi tu"

  Mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake Mh Daudi Yassin
 Makabidhiano


Wananchi na watendaji mbalimbali wilayani Makete Mkoani Njombe wameombwa kutoa ushirikiano kwa serikali iliyopo madarakani ili ilete maendeleo yaliyokusudiwa kwa taifa kama ilivyoahidiwa wakati wa kampeni

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Veronica Kessi wakati wa makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo aliyemaliza muda wake Mh Daudi Yassin hapo jana

Mh Kessi amesema kwa sasa ni muda wa kufanya kazi na si wakati wa siasa hivyo kwa ushirikiano wa pamoja kutawezesha wilaya ya Makete kusonga mbele kimaendeleo suala ambalo linahitajika katika serikali ya awamu ya 5

Mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake Mh Daudi Yassin amemueleza mkuu mpya wa wilaya kuwa wakati wa uongozi wake yapo baadhi ya mambo ambayo hakuweza kuyamaliza ingawa bado yanaendelea na utekelezaji ikiwemo maboresho ya shamba la mifugo la Kitulo, Mgogoro wa ardhi katika baadhi ya vijiji pamoja na matumizi ya soko lililopo Ngiu Makete mjini


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo