Kumbe Askofu Gwajima ni Mgonjwa.....Ashindwa Kutokea Mahakamani

PETER Kibatala wakili wa Josephati Gwajima Askofu wa Kanisa la ufufuo na uzima jana aliiomba mahakama kuahirisha tarehe ya kusikiliza kesi inayomkabili askofu huyo sababu anaumwa.
 
Kibatala alidai mahakamani Kisutu kuwa kutotokea kwa mteja wake jana kulitokana na yeye kuwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Wakili huyo  aliwasilisha madai hayo jana katika Mahakaama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Syprian Mkeha Hakimu Mfawidhi anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili Gwajima

Mahakama ilikubali ombi hilo na kwamba kesi hiyo itatajwa tena 2 Agosti mwaka huu.

Katika kesi hiyo Gwajima anadaiwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam.

Gwajima anadaiwa kufanya tukio hilo kati ya 16 na 25 Machi, mwaka 2015 katika Viwanja vya Tanganyika Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo