Vijana wakimbia kijiji chao kukwepa mafunzo ya mgambo


Vijana wa Kijiji wilayani hapa wamekimbia kijijini hapo kwa kile kinachodaiwa kukwepa mafunzo ya mgambo yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

George Twinzi mkazi wa kijiji hicho alisema vijana wameamua kukimbilia katika Miji ya Tunduma, Vwawa, Mlowo, Mbeya mjini na Makambako kukwepa kuandikishwa kushiriki mafunzo ambayo tayari zaidi ya vijana 100 wameandikishwa kushiriki.

“Mimi ni mmoja wa ambao wamejitokeza kushiriki mafunzo hayo bila shida kwa kuwa sioni sababu ya kukimbilia nisikokujua nikiacha shughuli zangu, wenzangu wengi wamekimbia wakidai  wanaogopa mateso ya kijeshi,” alisema Twinzi.

Ofisa Mtendaji Kata ya Kilimampimbi, Roland Mponzi alisema vijana waliokimbia kijiji hicho wametanguliza hofu inayotokana na masimulizi ya mafunzo ya mgambo ya zamani, lakini hivi sasa mafunzo hayo yameboreshwa si ya kutumia nguvu kama wanavyodhani.

Mponzi alisema ili kutoa hamasa kwa vijana wenzake, ameamua kujiunga na mafunzo hayo ili kuwa mfano.

Afisa Tarafa ya Vwawa, Haji Hamisi alikiri vijana kukimbia kijiji akisema hali hiyo inatokana na historia ambayo sasa haipo

Diwani wa Kata ya Kilimampimbi, Henry Mwilenga aliwashauri vijana waliotoroka kurudi kijijini hapo ili kupata mafunzo ambayo yanaweza kuwa msingi mzuri wa maisha yao kwa baadaye.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo