Maji yaadimika Tandala, Wananchi walazimika kukutana (Audio)

Uwepo wa tatizo la ukosefu wa maji katika vitongoji vya Singida na Posta kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe limelalamikiwa na wakazi wa vitongoji hivyo.

Wakizungumza nasi mara baada kumalizika kwa mkutano uliokuwa unajadili namna gani ya kutatua tatizo hilo, wananchi hao wamesema kuwa ukosefu wa maji umedumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa na kuwapelekea kutumia maji ya mtoni ambayo si salama kiafya.

Wamesema kuwa katika mkutano huo uliofanyika stendi mpya ya Tandala wamesikitishwa Na viongozi wa kitongoji na kijiji kushindwa kufika katika mkutano huo Licha ya taarifa za mkutano huo kuitishwa na viongozi hao

Akijibu tuhuma za kutofika kwenye mkutano huo pamoja na changamoto za maji mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Andowise Memba amesema ameshindwa kufika kwenye mkutano huo kutokana na mtendaji wa kijiji kwenda wilayani Makete kikazi na yeye kulazimika kubaki ofisini kuhudumia wananchi waliokuwa wakihitaji huduma mbalimbali za kiuongozi.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Tandala Mh, Egnatio Mtawa akizungumza na Green fm kwa njia ya simu amesema yeye kama diwani analijua tatizo hilo na tayari ameanza kulishughulikia na kilichochelewesha ni mabadiliko ya mfumo wa fedha za serikali ambapo kwa kuwa huu ni mwaka mpya wa fedha ni lzima kutakuwa na mabadiliko ya kimfumo huku akiwapa pole wananchi hao.
Na Asukile Mwalwembe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo