Ihela Hakuna cha Wanawake wala Wanaume, Wote ni kazi Tu

 Wananchi wa Ihela wakiwa kazini
 Muonekano wa jengo la zahanati Kijiji cha Ihela
Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuonesha ushirikiano katika kutekeleza shughuli za maendeleo katika maeneo yao kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuharakisha maendeleo katika maeneo yao

Kauli hiyo imetolewa na wananchi wa kijiji cha Ihela kata ya Tandala wilayani Makete wakati wakishiriki kufanya shughuli za maendeleo katika zahanati ya kijiji hicho ambayo bado inaendelea na ujenzi

Wananchi hao walikuwa wakiongeza uwanja wa zahanati hiyo kwa kuchimba gema lililopo jirani na zahanati ili kuweka uwazi, kazi ambayo waliisitisha kupisha mwenge wa uhuru kuweka jiwe la msingi katika zahanati hiyo Juni 16 mwaka huu

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Soniphei Sanga amewashukuru wananchi hao waliojitokeza kushiriki zoezi hilo na kuongeza kuwa wanatarajia kulikamilisha ndani ya mwezi Julai mwaka huu na ndipo waendelee na shughuli nyingine za kimaendeleo kijijini hapo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo