Chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa Rukwa kimeunga mkono
maamuzi yaliyotolewa na chama hicho makao makuu pamoja na yale yaliyokuwa
yakifanywa na wabunge wa upinzani katika bunge lililomalizika hivi karibuni
Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Rukwa Sabriki Malila
amesema hali na mwenendo wa kisiasa hapa nchini sio mzuri hali inayogandamiza
demokrasia na mfumo wa vyama vingi
Naye katibu wa CHADEMA wilaya ya Sumbawanga Pius Ngurumali amesema viongozi
na wanachama wa chama hicho hawatashiriki shughuli zozote za kiserikali ikiwemo
zoezi la kuapishwa kwa wakuu wa wilaya pamoja na lile la mwenge wa uhuru
unaotarajiwa kuingia mkoani humo kesho Julai 6 mwaka huu