Ajali mkoani Lindi, Jionee hapa

Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine amejeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Kilwa mkoani Lindi baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso.

Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Lindi imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kisangi katika kijiji cha Mkwanyule kwenye barabara ya Kilwa Lindi ambapo gari yenye nambari za usajili T 556 Suzuki Carry iliyokuwa ikiendeshwa na dereva Hijra Said Abdurahman ambae alifariki hapohapo baada ya gari yake kugongana uso kwa uso na gari nyingine Toyota Corolla yenye nambari za usajili T 840 Bug iliyokuwa inaendeshwa na Ahmad Mohamed Mfaume ambae amejeruhiwa katika paji lake la uso.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai amezungumzia kuhusu ajali hiyo na akatoa wito kwa madreva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kukomesha matukio ya ajali za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara na kusababisha vifo vya raia na uptevu wa mali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo